Bodi
ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF ), imefungua kesi ya madai
dhidi ya wanachama wake nane akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Magdalena Sakaya
Kesi
hiyo imefunguliwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikitaka
wanachama hao wasijihusishe na harakati zozote za chama hicho.
Mbali
ya Sakaya ambaye pia ni mbunge wa Kaliua mkoani Tabora, wadaiwa wengine
ni Thomas Malima, mbunge wa Mtwara Mjini,Mafta Nachumu, Omar Mhina
Masoud, Abdul Kambaya, Salama Masoud, Zainabu Mndolwa na Jafari Mneke.
Maombi
hayo mbayo yametajwa mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri
yamewasilishwa na Wakili wa bodi, Hashim Mziray na yamepangwa
kusikilizwa kesho.
Katika
maombi hayo yaliyopewa namba 1 ya mwaka 2017, bodi inaiomba mahakama
kutoa zuio kwa wadaiwa kutojihusisha katika masuala yeyote yanayohusiana
na chama hicho.
Mbali
ya maombi hayo, pia Wakili Mziray amewasilisha maombi madogo ya kuiomba
mahakama kuwaamuru wadaiwa wasijihusishe na mikutano ya chama hicho.
Aidha,
Mziray aliomba maombi yao madogo yasikilizwe kwa upande mmoja wa wadai
tu kwa kuwa wamechelewa kuwapatia nyaraka za madai yao wadaiwa.
"Mheshimiwa
tunaomba tusikilizwe upande mmoja ukizingatia maombi yameletwa chini ya
hati ya dharula na kwa mujibu wa sheria mahakama hii... inayo mamlaka
ya kufanya hivyo".
Hakimu Mashauri alisema anakubaliana na upande wa wadai na maombi hayo yatasikilizwa kesho mahakamani hapo.
Hatua
ya Bodi ya CUF, kukimbilia mahakamani inakuja ikiwa ni siku moja baada
ya upande unaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif
Shariff Hammad kupinga uteuzi wa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa
Ibrahim Lipumba.
Uteuzi
wa Profesa Lipumba ambao unapingwa ni ule alioufanya Machi 6, mwaka huu
baada kuwaondoa katika nafasi zao, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi,
Omar Ali Shehe.
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, Salim Abdull Bimani, Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi, Abdullah Bakar Hassan.
Wengine
ni Pavu Juma, Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadam na Sheria, Mahmoud
Ali Mahindo na Katibu wa Jumuiya ya Vijana, Yusuph Salim.
No comments:
Post a Comment