Chama cha Wananchi (CUF) kimedai kuna mipango inayofanyika ya kumvua
ukatibu mkuu Maalim Seif Sharif Hamad kwa sababu anaonekana kama kikwazo
cha utulivu Zanzibar.
Katika taarifa iliyotolewa na chama hicho jana, ilidai kuna kikao cha
chini chini ambacho kimeandaliwa na baadhi ya wajumbe wa upande mmoja wa
CUF, kikiwa na lengo hilo huku upande wa pili ikipinga kikao hicho
ambacho hakitambuliki kikatiba.
“Kwa mujibu wa katiba ya CUF Ibara ya 84 (1) ikisomwa pamoja na ibara ya
93 (1)(d) inaeleza kuwa; ...kutakuwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa
ambayo itakutana mara moja kwa kila miezi miwili,” ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilitolewa jana na Katibu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi
na Mawasiliano ya Umma, Mbarara Maharagande ilieleza mara ya mwisho
kikao cha kawaida cha Kamati ya Utendaji ya Taifa kilifanyika Februari
2, 2017 katika ofisi ndogo ya chama Vuga, Mjini Unguja.
No comments:
Post a Comment