MKAZI wa Kijiji cha Tatanda Kata ya Sopa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa,
Winfrida Silukala (54), amekufa baada ya kusombwa na maji kufuatia mvua
zinazoendelea kunyesha mkoani humu.
Winfrida alisombwa na maji juzi mchana wakati akitoka shambani akielekea nyumbani kwake baada ya mvua kunyesha mfululizo ikiwa imeambatana na upepo wa wastani.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Stephen Silupumbwe, mkazi wa kijiji hicho, alisema walimuona Winfrida akijaribu kujiokoa wakati akisombwa na maji, lakini bila mafanikio.
"Nami nilipiga kelele kuomba msaada na baadhi ya watu walifika na kumuopoa lakini alikuwa tayari amekwisha fariki dunia," alisema Silupumbwe.
Alisema wananchi kwa kushirikiana na serikali ya kijiji,walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ambao walifika eneo la tukio wakiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama chini ya Katibu Tawala.
Akizungumza na wananchi jana baada ya kutokea kwa maafa hayo, Katibu Tawala wilayani humu, Frank Schalwe, aliwataka wananchi kuwa waangalifu wanapokwenda mashambani kufanya shughuli zao za kilimo hasa wanapoona dalili za mvua kunyesha ili kuondokana na maafa kama hayo.
Aidha, Schalwe alisema Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humu, inaendelea kufanya tathmini kila kijiji kujua madhara yaliyotokea kufuatia mvua zinazonyesha mfululizo ili kuona namna ya kusaidia

No comments:
Post a Comment