Friday, February 3, 2017

YANGA YAPANIA KUENDELEZA LIGI KUU


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara Yanga leo wanashuka dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kupambana na Stand United ya Shinyanga huku akiahidi kufanya vizuri ili kuendelea kujiweka kileleni mwa ligi hiyo.

Akizungumza na Hotmix Michezo Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema, anaamini kikosi kipo imara kwa ajili ya mchezo huo ambao kwa upande wao ni mgumu na unawalazimu kushinda ili kupata pointi tatu huku akiwataka wanachama kuwa na umoja ili kuendelea kuipa timu sapoti katika michuano ya ligi pamoja na klabu bingwa Afrika ambayo inaanza hivi karibuni.

Mkwasa amesema, ligi inazidi kuwa ngumu katika mzunguko wa lala salama kutokana na kila timu kuhitaji kubaki katika nafasi nzuri huku akiongeza kuwa katika kila mchezo hususani kwa mchezo wa leo watacheza kwa kuhakikisha wanaibuka na ushindi ili kuweza kuhakikisha wanakuwa juu zaidi na kuwaacha mbali zaidi kwa pointi timu ya Simba SC.

No comments:

Post a Comment