Thursday, February 16, 2017

WAZAZI WACHUNGUZENI WATOTO WANAPOZALIWA MMOJA APOKELEWA MUHIMBILI HANAAA NJIA YA UKE

Dar es Salaam. Daktari Bingwa wa Upasuaji Watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Zaitun Bokhary amesema hivi karibuni wamempokea mtoto wa miaka miwili akiwa hana njia ya uke.
Dk Bokary amesema hospitalini hapo wanapokea watoto wenye matatizo hayo kati ya saba na nane kwa mwezi, ambao hufikishwa wakiwa wamecheleweshwa kiasi cha hata wakipata matibabu uwezekano wa viungo vyao kufanya kazi vizuri unakuwa mdogo.



Amesema matatizo hayo yanatokana na wazazi kutokuwa makini na viungo vya watoto wao wanapozaliwa.

“Wengi tunawapokea wakiwa na umri wa miaka saba mpaka 10, kwa mfano huyu mtoto ambaye hana njia ya uke kwa sasa ni vigumu kumfanyia upasuaji mpaka atakapofikisha umri wa balehe ndiyo itakuwa rahisi,” amesema.

Aliwataka wazazi kuwachunguza watoto wao kwani wengi wanazaliwa wakiwa na maumbile tofauti na kwamba, wamekuwa wawakipokea wengi wenye matatizo katika njia ya uke, uume na haja kubwa.

No comments:

Post a Comment