Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei, amesema miongoni mwa watuhumiwa hao 66, wamekamatwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Morogoro, kufuatia msako ulioendeshwa na jeshi hilo, ambapo kati yao, wamo waliokamatwa na viroba 21 vya bangi waliyokuwa wakiisafirisha kwenye gari aina ya noah huko kijiji cha Lubungo, Mikese na mmiliki wa gari hiyo Hamad Hassan mkazi wa Mbezi Luis jijini Dar es Saalam amekamatwa akihusishwa na tukio hilo, na watuhumiwa wengine watano wakazi wa Mlandizi na kiluvya wakikamatwa na bangi viroba 18 katika milima ya Lumba wakielekea Kibaha.
Kamanda Matei amesema watuhumiwa wengine watano, wamekamatwa kwa nyakati tofauti katika kijiji cha Mikoleko tarafa ya Mang’ula wilayani Kilombero wakiwa na vipande 28 vya nyama ya boko waliyokuwa wamehifadhi kwenye mfuko wa sandarusi maarufu kama safleti na kwenye ndoo ndogo ndani ya gunia la Mpunga huku mwingine akikamatwa na miguu miwili ya mbele ya swala, mikia miwili ya ngiri na nyanya za kutegea wanyama hao kwenye mfuko wa sandarusi huko Mbwade wilayani Morogoro.
Msako huo pia umeweza kukamatwa kwa mtuhumiwa mwingine ailiyekutwa na lita 100 za gongo huko kitongoji cha Mahamba, tarafa ya Kimamba, na mwingine akikutwa na bunduki aina ya gobole nyumbani kwake bila kibali huko Lubumu, tarafa ya Kidugalo, ambapo kamanda huyo wa polisi ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kuwafichua wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment