Moja
ya magazeti ya leo yamechapisha habari inayomtaja mbunge huyo
kujihuisha na bishara ya dawa za kulevya ambayo imekuwa ikipigwa vita
kila kona ya nchi kutokana na kupoteza nguvu kazi ya taifa.
Gazeti
hilo limeandika kuwa, jina la Ridhiwani limetajwa katika orodha ya
watuhumiwa wa dawa za kulevya na kuwa uchunguzi utafanyika. Pia limesema
mbunge huyo ametoa kauli nzito kwa hadhara.
Kiongozi
huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa, hafanyi biashara
hiyo haramu wala hakuwahi kufikiria kuifanya na kwamba nafsi yake i
tayari kufa masikini kuliko kupata utajiri kupitia njia hiyo.
Aidha,
ameeleza kuwa, anaamini kwamba uchunguzi utafanywa ili kuweza kuweka
mambo sawa kwani yeye hana kitu chochote cha kuficha.
Amesema kwamba, maneno hayo ya shutuma juu yake ni ya uongo na kwamba yametolewa na watu wasiomtakia mema na wasio na haya.
1. Tuhuma hizi za uongo kunihusisha na biashara haramu, isiyojali utu na kesho ya taifa ni maneno ya wasionitakia mema na wasio na haya.
-
2. Ni jambo jema na faraja kubwa kwangu kama uchunguzi unafanywa kuhusu tuhuma hii. Niukombozi kwangu kwani kweli daima huweka watu huru.3. Sifanyi biashara hiyo haramu wala sijawahi kufikiria kufanya. Nafsi i radhi kufa maskini kuliko kutafuta utajiri kwa njia hiyo.
No comments:
Post a Comment