Mwenyekiti wa bodi ya Parole, Augustine Mrema amesema kuwa vita dhidi ya
biashara ya dawa za kulevya itasaidia kupunguza kwa wingi wa wafungwa
magerezani kwakuwa watu wengi watakapoacha kujihusisha na biashara hiyo
vitendo vya uhalifu navyo vitapungua.
Akitoa tathmini ya utendaji wa bodi hiyo jijini Dar es Salaam, Mrema ametoa wito kwa Watanzania wote kwa kutumia majukwaa mbalimbali kukemea matumizi na biashara ya dawa za kulevya .
Mrema alisema, “Wasiruhusu rais kushindwa hili au Makonda kushindwa hili, hatutakaa tuibuke tena ni kukamatia hapohapo kwahiyo watu wema wajitokeze katika hii vita wasimuachie rais peke yake wasimuachie Makonda na Simon Sirro, tujitokeze tuhakikishe huu mtandao unavunjwa.”
Aliongeza “Mimi nilikuwa napendekeza kwamba kila mkutano wa hadhara utakaofanywa na viongozi wa vyama wasiache hii agenda tukiendelea hivyo watashindwa, tumeona tu kelele kidogo dawa zimekosekana mtaani, Je tukikazana baada ya mwezi madawa yatakuwa ni historia, alihoji?”

No comments:
Post a Comment