Wednesday, February 15, 2017

MGODI MWINGINE KUFUKIA WATU MARA


Taarifa kutoka Butiama kwenye Mkoa wa Mara leo ni kuhusu miili ya watu wawili kupatikana February 14 2017 kwenye Mgodi wa Buhemba ambapo kwa taarifa za awali watu 13 wameokolewa wakiwa wamejeruhiwa baada ya kufukiwa ndani ya mgodi.
Kutoka kwenye eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya ya Butiama Annarose Nyamubi amesema “Ni kweli kabisa kwenye Wilaya ya Butiama Magunga ulipo mgodi wa zamani wa dhahabu wa Buhemba shimo moja limefukiwa na kifusi saa 3 asubuhi”

“Mpaka saa 7 mchana tuliweza kuokoa watu 13 na wengine wanaendelea na matibabu huku wengine wakiwa wameruhusiwa wako nyumbani, kuna Wachimbaji wengine wanne bado wanatafutwa na idadi inaweza kuongezeka”

“Idadi inaweza kuongezeka kwasababu kuna Wachimbaji ambao huwa wanazamia bila kujisajili majina yao kabla ya kuingia mgodini, wale ambao huwa wanajisajili ndio rahisi kutambua rekodi zao… tunavyoendelea na zoezi” – DC Annarose

No comments:

Post a Comment