Nyota wa Barcelona Lionel Messi na Neymar wanaweza kunyimwa nafasi ya
kuingia Uingereza iwapo watafuzu kuingia kwenye hatua inayofuata na
kufuzu fainali kutokana na kesi zinazoendelea za makosa ya ukwepaji
kodi.
Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin amesema kuwa anahofia wachezaji hao
wanaweza wasiweze kuingia Cardiff ambapo mchezo wa fainali wa UEFA mwaka
huu utafanyika kwenye uwanja wa Principality Stadium mwezi Juni iwapo
tu watafanikiwa kufuzu.
Hata hivyo itakuwa kama maajabu Barcelona kuingia kwenye fainali ya
mwaka huu ya mwezi Juni kwani tayari wameshafungwa mabao 4-0 kwenye
mchezo wa kwanza wa raundi ya 16 dhidi ya Paris Saint-Germain.
Mapema msimu huu, beki wa PSG, Serge Aurier alinyimwa ruhusa ya kuingia
Uingereza kwenye mchezo dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Emirates mwezi
Novemba kutokana na kuwepo kwenye rufani ya kesi ya kudhuru.
Lakini pia hali ya kisiasa inayohusu mpango wa Brexit ikiendelea kuwepo,
Ceferin anaamini kuwa England itakumbana na tatizo kubwa kwenye mpango
wa kutaka kuandaa mashindano ya Mataifa ya Ulaya mwaka 2028 au kombe la
Dunia mwaka 2030.
No comments:
Post a Comment