Muda
mfupi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutaja
orodha ya majina 65 ya watuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za
kulevya, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeibuka na
kukosoa utaratibu unaotumiwa na kuongozi huyo.
CHADEMA
kimekosoa utaratibu unaotumiwa wa kutangaza majina hadharani ambapo
wamesema kuwa baadhi ya wanaotajwa ni viongozi wa ngazi za juu wa
kitaifa.
Mkutano
huo ulioongozwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt Vicent Mashinji umekuja
saa chache baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe kutajwa
miongozi mwa watuhumiwa hao 65.
“Majina
mengi yaliyotajwa kuna jina la Mwenyekiti wa chama Mbowe, suala la
utetezi wake au maelezo hilo ni suala binafsi sababu kilichotajwa ni
jinai lakini kimsingi tunachukua nafasi hii kulaani jinsi tusivyoweza
kuendesha utawala wa sheria kwenye nchi yetu na jinsi tusivyofuata
kanuni zilizowekwa dhidi ya sheria.
"Mh.
Mbowe ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani
bungeni, ni Mbunge wa Hai…. kwahiyo kuna taratibu za kufata unapokua na
kusudio la kumuita.”
Katibu
huyo alisema kuwa si sahihi kutaja majina ya viongozi wakubwa hadharani
kwa tuhuma tu ambazo hata hazijathibitishwa. Dkt Mashinji amesema kuwa
huko ni kukosa utashi na busara za uongozi.
Katika
orodha hiyo ya awamu ya pili iliyotolewa na RC Makonda leo mchana
imejumuisha viongozi wengine kama, Askofu Josephat Gwajima, Mwenyekiti
wa Yanga, Yusuf Manji, Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan
No comments:
Post a Comment