Wednesday, February 8, 2017

MAKONDA KATAJA MAJINA MENGINE 65 YA WANAOHUSIKA NA MADAWA YA KULEVYA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametaja majina ya watuhumiwa wengine 65 wa madawa ya kulevya, wakiwemo Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Elikael Mbowe, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, Askofu Josephat Gwajima na Mbunge Mstaafu wa Kinondoni, Idd Azzan.

Makonda amesema hii ni awamu ya pili ya oparesheni ya kusaka watuhumiwa wa mtandao wa biashara haramu ya madawa ya kulevya, ambapo amesema awamu hii itakuwa ngumu ikilinganishwa na ile ya kwanza iliyohusisha polisi na wasanii kukamatwa.

Makonda amewataka watu wote 65 waliotajwa, kuhakikisha wanaripoti kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam (Sentro) siku ya Ijumaa saa 5 asubuhi kwa mahojiano zaidi.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake, Makonda amesema kuwa, waliokamatwa awali ndiyo waliofanikisha kupatikana kwa orodha hiyo mpya.

No comments:

Post a Comment