Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma amewathibitishia mashabiki wa klabu
hiyo hatacheza mechi ya Jumamosi dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Ngoma amewambia mashabiki mubashara kupitia mtandao wake wa Facebook alipokuwa akifafanua habari kwamba amegoma kucheza.
"Wengi wanauliza kuhusiana na hali yangu, ukweli ni kwamba mimi ni
majeruhi na sitacheza mechi ya Jumamosi, siwezi kucheza kwavile bado
nina majeraha."
Kuna watu wanazusha kwamba nimegoma kucheza, hakuna kitu kama hicho hayo
ni maneno tu, mimi ninaumwa ntachezaje? mnatakiwa kuelewa afya ya
mchezaji ni kitu muhimu kwenye maisha ya mpira.
"Nitakuwa nje ya uwanja kama wiki sita, wala mashabiki wasiwe na
wasiwasi kuna Chirwa(Obrey) na Tambwe (Amissi) ni wanajeshi watapambana.
Timu itafanya vizuri."
No comments:
Post a Comment