Shughuli
za ujenzi wa jengo jipya la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam (Terminal 3) jana tarehe 09 Februari, 2017
zimeendelea kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli aliyefanya ziara ya kushtukiza jana tarehe 08
Februari, 2017.
Wafanyakazi
850 wameendelea na kazi mbalimbali za ujenzi wa uwanja huo ikiwa ni
pamoja na ujenzi wa njia za kuingia na kushuka kwenye ndege, mifumo ya
ujazaji wa mafuta ya ndege, maeneo ya kuegeshea ndege, sehemu ya kuingia
na kutoka jengoni, mifumo ya viyoyozi na ujenzi wa nguzo.
Pia,
timu ya wataalamu wanaosimamia ujenzi huo imefanyiwa mabadiliko ambapo
wataalamu wengine 9 kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
wamepelekwa na kuanza kazi mara moja.
Mkandarasi
ambaye ni kampuni ya BAM International ya Uholanzi, Mhandisi Mshauri
ambaye ni kampuni ya ACE ya Misri na wafanyakazi walioajiriwa katika
mradi huo wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli kwa hatua alizochukua zilizowezesha shughuli za
ujenzi kuendelea.
Katika
ziara ya juzi, Mhe. Rais Magufuli alielezea kusikitishwa na utekelezaji
wa mradi huo uliopangwa kugharimu Shilingi Bilioni 560 kiasi ambacho ni
kikubwa mno ikilinganishwa na jengo linalojengwa na Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa alikiri kuwepo kwa
dosari na kuahidi kuchukua hatua.
Mhe.
Rais Magufuli ameahidi kuwa Serikali inafanya juhudi za haraka kutoa
malipo ya Mkandarasi na Mhandisi Mshauri yaliyosababisha kusitishwa kwa
ujenzi.
No comments:
Post a Comment