Rapper Joh Makini kutoka kundi la Weusi, amefunguka kuhusu kufikiria kuacha muziki na kufanya ishu zingine.
Joh amesema hayo Jumatatu hii kwenye kituo cha radio cha EA Radio ambapo alipata fursa hiyo kwenye siku hiyo ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa huku akiongeza kuwa haitokuja kutokea maishani mwake, kuacha kurap labda kifo ndio kiwe sababu ya yeye kumtenganisha na muziki.

“Kufanya vitu vingine tofauti katika maisha hilo ni muhimu kabisa, lakini kufikiria kuacha muziki sijui, kwa sababu nakuwa mzito sana kusema itafikia siku nitashindwa kurap?, Sijui ila napenda muziki sana”, amesema Joh Makini.
“Endapo ikitokea nikiacha kurap na kutoenda studio lazima nitakuwa kwenye mzunguko wa kufanya vitu vingine na muziki pia. Sioni sababu ya kuacha muziki labda kifo ndio kitanitenganisha lakini sio kitu kingine,"ameongeza.
Joh ameendelea kusema kuwa kwa sasa muziki wa Hip Hop nchini unalipa kwa kiasi kikubwa, tofauti na ulivyokuwa zamani huku akiwarushia dongo wasanii wanaolalamikia kuwa yawezekana wao wenyewe hawajajipanga katika kutoa kazi nzuri ndio maana wanayumba.
No comments:
Post a Comment