Beki wa kati wa klabu ya Yanga leo anatarajiwa kuanza mazoezi leo ikiwa ni takribani mwezi mmoja upite tangu agome akidai stahiki zake.
Yondani alikuwa hashiriki katika mazoezi ya Yanga chini ya Kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera akidai fedha zake za mshahara pamoja na hitaji la mkataba mpya.
Baada ya kugoma kwa muda wote huo, wadau wa Yanga wakongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum kuivusha klabu hiyo wakati wa mpito, Abbas Tarimba, walikutana na Yondani kuweka mambo sawa.
Katika kikao walichokaa pamoja na Yondani, imefahamika wamefikia pazuri na mchezaji huyo na leo anatarajiwa kuanza mazoezi kujiwinda dhidi ya Gor Mahia FC kuelekea mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa Julai 29 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Imeelezwa baada ya kukutana na Tarimba, tayari Yondani ameshakubaliana kila kitu na Yanga ikiwemo suala la kuongeza mkataba mpya pamoja na malipo ya stahiki zake zote.

No comments:
Post a Comment