Waziri wa zamani Christopher Chiza ni miongoni mwa wana CCM, walioonyesha nia ya kuwania jimbo la Buyungu lililoachwa wazi baada ya mbunge wake, Kasuku Bilago kufariki dunia. Bilago alifariki dunia Mei mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Chiza aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo hilo kuanzia Desemba 2005 hadi Julai 2015 ambapo alimwachia Bilago. Aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji kuanzia February 13, 2008 hadi Novemba 28, 2010, Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika kuanzia Novemba 28, 2010 hadi Mei 7, 2012, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika kuanzia Mei 7, 2012 hadi Novemba 5, 2015.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kakonko, Abdul Kambanga amesema hadi kufikia Julai 3, jumla ya wana CCM 20 wamechukua fomu kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mdogo ujao.
Wana CCM wengine waliochukua fomu ni pamoja Jeremia Ruhele, Maganga Toga Manyama, Brighton Gwamagobe, Mawazo Methusela, Hekima Ngeza, Baraka Mathias, Leopold Muhagaze, Emmanuel Gwegenyeza, Aloys Kamamba na Marco Kumdanko.
Wengine ni Jiles Damianna, Olaf Kaboboye, Aram Kingo, Liberi Ndabita, Ernest Basaya, Msakila Kabende, Anthon Fumbe, Daudi Kidyamali na Meshack Abednego.
kwa mujibu wa katibu huyo, wana CCM wanatarajia kupiga kura Julai 6 ili kumpata mgombea atakayechuana na wagombea wa vyama vingine katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu.

No comments:
Post a Comment