Tuesday, July 10, 2018

CAF YAMFUNGIA MAISHA MWAMUZI MLA RUSHWA KUTOKA KENYA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limemfungia maisha mwamuzi wa Kenya, Aden Marwa baada ya kugundulika amepokea hongo (rushwa) nchini Urusi.

Marwa raia wa Kenya amekutana na kimbembe hicho baada ya kuingia kwenye mtihani huo baada ya kunaswa kwenye kipande cha video kinachomuonesha akipokea pesa kutoka kwa mwandishi wa habari kabla hata kuanza kwa michuano ya kombe la dunia.

Baada ya uchunguzi huo uliyofanywa na Anas, ulimthibitisha Marwa kufanya kitendo hicho na hivyo kuondolewa.

Kutokana na tukio hilo haibu Marwa ambaye alikuwa mwalimu wa shule ya sekondari ya Komotobo iliyopo Kuria East, Migori mwa Kenya ameamua kuachana na taaluma hiyo.

Mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 41 ambaye alikuwa mwalimu wa masomo ya Mathematics na Chemistry alipokea rushwa ya dola za Kimarekani 600 sawa na (Sh60,000) za Kenya.

Familia ya mwamuzi huyo ambaye pia alipata bahati ya kupuliza kipyenga mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil imekuwa ikikataa kupokea wageni wowote wanao watembelea kutokana na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment