WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Augustine Mahiga, amesema ufunguzi wa Kituo cha Taaluma za China (CCS) kilichopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam utaimarisha ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya nchi hizo.
Aidha, Waziri Mahiga aliwataka Watanzania kutumia (CCS) kujifunza mbinu ilizotumia China kupiga hatua kubwa kimaendeleo kwa muda mfupi.
Alisema kupitia kituo hicho cha China, UDSM itanufaika kwa kutoa elimu, kufanya tafiti na kukuza utekelezaji wa mahusiano ambayo viongozi waasisi wa nchi hizo walianzisha.
Dk. Mahiga aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizindua kituo hicho na kueleza kuwa China imepiga hatua kimaendeleo hivyo ni fursa ya pekee kwa Watanzania kubadilisha mtazamo kwa kujifunza kupitia nchi hiyo.
Walezi wa kituo hicho ni Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke.
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya wadhamini ya kituo hicho inayoongozwa na Prof. Rwekaza Mukandara ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi na Balozi wa Tanzania Italia wa zamani, Prof. Costa Mahalu.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Dk. Mahiga alitaka kituo hicho kiwe chachu kwa Watanzania kujifunza tamaduni za Kichina ambazo zimesaidia nchi hiyo kufikia maendeleo kwa muda mfupi.
Dk. Mahiga alisema UDSM itanufaika na uwepo wa kituo hicho ambacho kitatumika kwa ajili ya kusomesha, kufanya tafiti na kukuza utekelezaji wa uhusiano ambao viongozi wameingia baina ya nchi hizo mbili.
Alisema madhumuni ya kituo hicho ni kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili, kufanya tafiti katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi, ustawi wa jamii na kutazama uhusiano wa elimu na utamaduni.
"Upo uhusiano mzuri kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na China hivyo hatua ya kufungua kituo hiki ni ubunifu wa hali ya juu kwa uongozi wa UDSM hasa kwa Mkurugenzi wa kituo hiki, Prof. Humphrey Mushi," alisema.
Dk. Mahiga alisema uwepo wa kituo hicho ni nafasi ya pekee Tanzania kutazama chimbuko, misingi ya uhusiano na historia kati ya nchi hizo mbili.
"Misingi ya China ya uhusiano ni kuheshimu mipaka, kutokuingilia siasa za ndani, kutogombana na majirani na kuishi vizuri kwa ushirikiano wa kibiashara na katika miaka ya hivi karibuni wameongeza kigezo kingine ambacho ni mkanda na barabara maana yake kuongeza uhusiano wa karibu zaidi na nchi duniani," alisema.
Balozi Mahiga alisema Tanzania kupitia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere iliisaidia China kurudi katika Umoja wa Mataifa baada ya hotuba yake kwenye Baraza Kuu la UN iliyojenga hoja za umuhimu wa China kundini humo.
"Fadhila ambayo Mwalimu Nyerere aliitoa bado China wanailipa bila masharti na inajionyesha katika biashara, uwekezaji na sasa hivi uwekezaji katika viwanda ambayo nchi hiyo ni ya pili ikifuatiwa na Uingereza, Afrika Kusini," alisema.
Pia alisema ipo misaada ya moja kwa moja ambayo China inaipatia Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwamo kilimo, afya, elimu na miundombinu.
Kwa upande wake, mlezi wa kituo hicho, Mizengo Pinda alisema mambo ambayo Tanzania inatakiwa kujifunza kupitia China ni nidhamu ya utumishi wa umma katika kusukuma gurudumu la kufikia maendeleo.
"Rais John Magufuli amekuwa akipiga kelele 'hapa kazi tu' na ukienda China ndipo utakapoona kazi ni kufa na kupona," alisema Pinda aliyekuwa Waziri Mkuu 2008-2015. "Hakuna utani katika hili na wanajisimamia kwa karibu kuhakikisha wanapiga hatua ya maendeleo."
Pinda alitaja jambo lingine kuwa ni kupiga vita rushwa na kueleza kuwa China wanazingatia uadilifu wa viongozi waliokabidhiwa madaraka.
"Lazima kilimo kiwe nyenzo ya kuleta mabadiliko ya haraka na elimu itiliwe msisitizo kuanzia awali hadi ngazi ya juu na ihusiane na maendeleo ya eneo husika."
Naye mjumbe wa bodi ya wadhamini ya kituo hicho, Dk. Mengi aliwataka Watanzania wajiamini na kuwa na macho yanayoona fursa.
"Kituo hiki kinachozinduliwa leo lazima kiangalie changamoto hizi mbili ambazo zinawakabili Watanzania walio wengi ambazo ni kutojiamini na macho yanayoona fursa," alisema Dk. Mengi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP.
"Nilikwenda China na Waziri Mkuu mstaafu Pinda, sikuona Wachina wanaotembea taratibu barabarani, wenzetu wanajali muda, lazima Watanzania tujali muda."
Balozi wa China Ke, alisema kituo hicho kimekuja wakati mwafaka na kitaleta mchango wa kipekee na muhimu katika kuitambulisha China hapa Tanzania.
Pia alisema kitasaidia kufanya tafiti za kina katika masuala mbalimbali yanayoonyesha uzoefu na maendeleo ya China kwa ajili ya manufaa ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.

No comments:
Post a Comment