Saturday, May 12, 2018

KOREA KASKAZINI KUSAIDIWA KIUCHUMI NA MAREKANI

Marekani imesema itaisaidia Korea Kaskazini kiuchumi endapo Pyongyang itaachana na mabomu ya nyuklia.

Hayo yamezungumzwa baada ya Mike Pompeo kufanya ziara nchini Korea Kaskazini.

Kwa mujibu wa habari,waziri huyo amefanya mazungumzo ya kina na Kim Jong Un kuhusu uamuzi wa Marekani endapo nchi hiyo itaachana na makombora ya nyuklia.

Hapo awali rais Trump alitangaza rasmi kuwa mkutano baina yake na Kim unatarajia kufanyika 12 Juni Singapore.

Marekani imeahidi kufanya ushirikiano na Korea Kaskazini an Kusini endapo mkutano kati ya Kim na Trump utazaa matunda.

No comments:

Post a Comment