Mchezaji Mohammed Fakhi Gharib wa Kagera Sugar.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ya bodi ya Ligi.
Taarifa ambayo ilisambaa jana kutoka ndani ya Bodi ya ligi imeeleza kuwa bodi hiyo imefungua malalamiko kuyapeleka kwa Kamati ya Nidhamu ya TFF ambapo Mkemi anatakiwa kufika kesho kutwa Jumapili, saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Katika taarifa hiyo, imeelezwa kuwa Mkemi aliishutumu na kuidhalilisha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kamati ya Saa 72) ya Bodi ya Ligi kuwa inaendeshwa kwa unazi na imegubikwa na rushwa katika kushughulikia suala la kadi tatu za njano kwa mchezaji Mohammed Fakhi Gharib wa Kagera Sugar.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi.
Imeelezwa kuwa Bodi ya Ligi inataka Mkemi aadhibiwe kwa mujibu wa Ibara ya 53 (1) na (2) ya Kanuni za Nidhamu za TFF pamoja na Kanuni ya 41 (2) ya Ligi Kuu, pia apewe adhabu nyingine kama ambavyo Kamati ya Nidhamu itaona inafaa kwa kuzingatia Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.
Walipotafuta mabosi wa Bodi ya Ligi hawakupokea simu wakati Mkemi alipopigiwa alikuwa anakata.
No comments:
Post a Comment