Wednesday, April 25, 2018

SERENGETI BOYS KUCHUANA NA KENYA LEO

Timu ya Taifa ya Vijana U17 (Serengeti Boys) leo inatupa karata yake muhimu kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Kenya.

Mchezo huo utachezwa saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Muyinga nchini Burundi.

Kufuzu hatua ya nusu fainali Serengeti Boys walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda kwenye mchezo wa kwanza kabla ya kuifunga Sudan kwa magoli 6-0 kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B.

Tunaitakia kila la kheri Serengeti Boys iweze kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa nusu fainali.

No comments:

Post a Comment