Wednesday, March 7, 2018

JINSI UGONJWA WA FIGO UNAVOSABABISHA MATATIZO YA UZAZI KWA WAJAWAZITO


Wanawake wanaougua magonjwa ya figo hukabiliana na matatizo ya uzazi hasa kushindwa kushika mimba na hata kuharibika kwa mimba.

Kutokana na hali hiyo madaktari hulazimika kuwasaidia kukomaza mtoto iwapo mjamzito amekaribia kipindi cha kujifungua lakini pia kwa hali hiyo husababisha wengi huzaa mtoto njiti.

Daktari Bingwa wa Magonjwa wa Wanawake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Vincent Tarimo amesema hayo jana alipozungumza na chombo kimoja cha habari.

“Magonjwa ya figo kwa wanawake yanaweza kuwekwa katika makundi makubwa mawili, kuna yanayohusiana na ujauzito na yasiyohusiana na ujauzito ambayo yote huweza kuua,” alisema.

Alisema katika yale yanayohusiana na ujauzito tatizo la shinikizo la juu la damu ndilo ambalo huchochea zaidi figo kuathirika na kufa.

No comments:

Post a Comment