Theresa May akitia saini barua ya kuanza kujiondoa EU |
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametia saini barua ambayo
itaanzisha rasmi mchakato wa kuiondoa Uingereza kutoka kwa Muungano wa
Ulaya.
Barua hiyo inatoa taarifa rasmi ya kujiondoa kwa muungano huo kwa kitumia Kifungu 50 cha Mkataba wa Lisbon.
Itawasilishwa kwa rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk baadaye leo.
Kwenye taarifa kwa bunge la chini nchini Uingereza, Bi May baadaye
anatarajiwa kuwaambia wabunge kwamba hatua hiyo inaashiria "wakati we
taifa letu kuungana pamoja."
Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kura ya maoni iliyoandaliwa Juni
mwaka jana, ambapo wapiga kura waliunga mkono kujiondoa kutoka kwa EU.
Barua ya Bi May itawasilishwa kwa Bw Tusk Jumatano mwenzo wa saa sita
unusu adhuhuri saa za Uingereza na balozi wa nchi hiyo katika EU Sir Tim
Barrow.
Waziri mkuu ambaye ataongoza kikao cha baraza la mawaziri asubuhi,
baadaye atatoa hotuba rasmi kwa wabunge kuthibitisha kwamba mchakato wa
Uingereza kujiondoa EU umeanza.
Ataahidi "kuwakilisha kila mtu katika Uingereza yote" wakati wa
mazungumzo hayo - wakiwemo raia wa EU (wanaoishi Uingereza), ambao bado
haijafikiwa uamuzi kuhusu hatima yao baada ya Uingereza kujiondoa kutoka
kwa muungano huo.
"Nimejitolea kuhakikisha tunapata mkataba bora zaidi kwa kila mtu katika nchi hii," anatarajiwa kusema.
"Kwani, tunapokabili fursa na changamoto zilizopo mbele yetu, maadili
yetu ya pamoja, maslahi na ndoto zetu zinaweza - na ni lazima - zitulete
pamoja."
No comments:
Post a Comment