Serikali
imesema iko tayari kupokea ushauri wa namna bora yakuimarisha utendaji
wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kuwa azma ya Serikali ni
kuendeleza Taasisi hiyo kwani bado inahitajika na madhumuni ya
kuanzishwa kwake yana tija kwa Taifa.
Akizungumza
wakati akijibu Hoja za Wabunge na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma
na Maendeleo ya Jamii Waziri wa Elimu Sayansi na Teknplojia Profesa
Joyce Ndalichako amesema kuwa Bado Taasisi hiyo inahitajika hivyo
Serikali inaangalia namna ya kuiboresha na si kuivunja kama
ilivyopendekezwa.
“
Taasisi ya Elimu ilianzishwa kwa lengo la kutoa elimu kwa wale
waliokosa katika mfumo rasmi na pia kutoa mafunzo endelevu hivyo bado
kuna umuhimu wa kuendeleza Taasisi hii” Alisisitiza Prof. Ndalichako.
Akifafanua
Prof. Ndalichako amesema kuwa Taasisi hiyo inaweza kuimarishwa zaidi
ili kuendana na mahitaji ya sasa ikiwa ni sehemu ya mikakati ya
Serikali kuimarisha na kukuza kiwango cha elimu nchini.
Akizungumzia
mikakati yakuimarisha elimu nchini Profesa Ndalichako amesema kuwa kwa
sasa Serikali inafanya ukarabati wa Shule Kongwe hapa nchini, vyuo vya
Ualimu, na Ujenzi wa maktaba yakisasa katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 2500 kwa wakati mmoja
hiyo ikiwa ni sehemu ya miradi yakuboresha elimu inayotekelezwa na
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Maoni
ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii
yalipendekeza kuwa TEWW ivunjwe ambapo Serikali imesema kuwa Bado
Taasisi hiyo inahitajika na ina tija hivyo kitakachofanyika ni
kuiboresha zaidi ili kukuza elimu hapa nchini na Si kuivunja kama
ilivyopendekezwa.
Taasisi hiyo imeanzishwa kwa sheria namba 139 ya mwaka 1989 na iko chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.
No comments:
Post a Comment