Kwenye ukurasa wake wa instagram Sugu ameandika ujumbe akisema kwamba serikali iruhusu uchunguzi kutoka vyombo binafsi vya kimataifa, ili kuwatambua na kuthibitisha waliompiga risasi Tundu Lissu.
"Nami naunga mkono kuitaka serikali iruhusu uchunguzi wa kimataifa kutoka vyombo kama FBI au 'Scotland Yard' ili kuwatambua na kuwathibitisha waliohusika na kitendo hiki ili wawajibishwe kwa hili jaribio la mauaji lisilo na maana, na hao wasiojulikana sasa wajulikane", ameandika Sugu.
Pia kwenye ujumbe huo Sugu ameweka wazi kuwa alitakiwa kusafiri kwenda nchini China kikazi lakini amelazimika kusitisha safari hiyo kwa sababu ya matatizo ya Tundu Lissu
No comments:
Post a Comment