Thursday, October 5, 2017

WANAKIJIJI WAMUUA NA KUMLA CHATU INDONESIA BAADA YA VITA VIKALI

This handout picture taken on 30 September 2017 and released on October 4, 2017 by the Batang Gansal Police shows villagers beside a 7.8 metre (25.6 foot) long python which was killed after it attacked an Indonesian man, nearly severing his arm, in the remote Batang Gansal subdistrict of Sumatra island.
Chatu mkubwa alikumbana na kifo kibaya baada kwa kuuliwa, alilipopoteza vita vikali kwa mwanamume mmoja nchini Indonesia.
Mlinzi Robert Nababanm, alikumbana na chatu huyo kwenye shamba moja la michikichi wilaya ya Batang Gansal huko Sumatra Indonesia.
Bw Nababan akajaribu kumshika chatu huyo ambaye anaripotiwa kuwa wa urefu wa mita 7.8.Chatu huyo alimshambulia na wote hao wakamenyana hadi pale Bw. Nababan alipomuua chatu huyo akisaidiwa na wanakijiji.
Mlinzi huyo alinusurika na majeraha mabaya.
Hata hivyo chatu huyo hakubahati vile Bw. Nababan alivyobahatika, aliwekwa kwenye maonyesho kijijini, kabla ya kukatwa katwa, akakaangwa na kuliwa.

No comments:

Post a Comment