Mabingwa watetezi Real Madrid wakiwa nyumbani Santiago Bernabeu wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Apoel. Mabao mawili kati ya hayo yakifungwa na Cristiano Ronaldo na kumfanya kuwa mchezaji mwenye mabao mengi zaidi katika UEFA pekee akiwa na mabao 107.
Tottenham Vs Dortmund
Umahiri wa kane mbele ya goli ndio tofauti kubwa waliokuwa nayo Suprs ambao kwa kipindi kirefu cha mchezo huo walilazimika kulinda lango la kutokana na mchezo mzuri ulioonyeshwa na vijana wa Dortmund.
Bao lake la kwanza liliwawacha Dortmund bila jibu baada ya kutamba na mpira kutoka upande wa kushoto wa uwanja kabla ya kucheka na wavu dakika 15 katika kipindi cha kwanza baada ya bao la dakika ya 11 la Son Hueng-min kusawazishwa na mshambuliaji wa Dortmund Andriy Yarmolenko.
Bao la pili la Kane ulikuwa mkwaju wa kimo cha nyoka katika dakika ya sitini na hivyobasi kuipatia timu yake motisha ya kukabiliana na tishio la wapinzani wao waliotawala mechi hiyo.
Hatahivyo Tottenham walimaliza mechi hiyo wakiwa wachezaji 10 baada ya beki Jan Vertonghen kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumshika mchezaji wa ziada wa Dortmund Mario Gotze.
No comments:
Post a Comment