Sunday, September 17, 2017

MAJALIWA ATOA ONYO KALI KWA VIONGOZI SERIKALINI WASIO NA MASHAMBA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amepiga marufuku Viongozi wa Serikali wasiokuwa na mashamba ya mikorosho kutojihusisha na biashara ya uuzaji wa zao hilo.

Ametoa agizo hilo hii jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa korosho uliofanyika mkoani Tanga, ambapo amewataka viongozi hao kutoingilia biashara ya zao hilo kwakuwa haliwahusu.

“Kama huna shamba, huwezi kuwa na korosho, unauza umepata wapi. Jukumu lenu ni kufuatilia, kukemea na kuchukua hatua stahiki penye udhaifu na si vinginevyo,”amesema Majaliwa

Amesema kuwa kama viongozi hao wanahitaji kuuza korosho watumie muda huu ambao Serikali inahamasisha watu wafungue mashamba mapya nao watumie fursa hiyo na kulima.

Hata hivyo, ameongeza kuwa ni vyema kila mdau akahahakikisha anatimiza wajibu wake ipasavyo kama ni mkulima alime kwa kuzingatia stadi za kilimo na mnunuzi azingatie taratibu zilizopo.

No comments:

Post a Comment