GEORGE LWANDAMINA.
Kocha wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, George Lwandamina, amesema kuwa mechi dhidi ya Mtibwa Sugar itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Uhuru "si ndogo" kama ambavyo baadhi ya wadau wanavyoiangalia.
Akizungumza Lwandamina, alisema kuwa matokeo mazuri waliyonayo Mtibwa Sugar yanawasaidia kuondoa wasiwasi katika mechi itakayowakutanisha na hivyo anaamini itakuwa na changamoto zaidi kwa upande wake.Lwandamina alisema kuwa anaamini uzoefu wa mechi za kimataifa na faida ya kucheza nyumbani ndiyo vitu anavyovitegemea kumsaidia kupata ushindi katika mchezo huo.
"Mechi dhidi ya Mtibwa Sugar ni ngumu na ya ushindani, ni moja kati ya klabu zenye wachezaji wanaojua kupambana," Lwandamina alisema kwa kifupi.
Kocha huyo wa zamani wa Zesco ya Zambia aliongeza kuwa anaamini wachezaji wake watapambana, ili wapate pointi zote tatu katika mechi hiyo na kukaa katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.
Mzambia huyo alifurahi kuona mshambuliaji wake wa kimataifa, Amissi Tambwe, anaendelea vyema na uamuzi wa kumpanga utajulikana kesho baada ya kumaliza mazoezi.
No comments:
Post a Comment