Kuumia huko kulimfanya Tambwe kuikosa mechi hiyo pamoja na ile ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli FC ya Iringa ambazo zote Yanga haikuweza kufanya vizuri, kwani ile ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, ilifungwa na ile ya ligi kuu dhidi ya Lipuli iliambulia pointi moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1.
Tambwe amesema kuwa hivi sasa anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu na tayari ameshaanza kufanya mazoezi mepesimepesi anayoyafanya chini ya jopo la madaktari wa timu hiyo katika gym lakini pia ufukweni.
Alisema ana hasira ile mbaya na timu ya Simba na anaipa mechi saba za kuongoza ligi ambazo ni sawa na dakika 630, baada ya hapo Yanga itachukua usukani mpaka mwishoni mwa msimu huu.
“Namshukuru Mungu naendelea vizuri na tayari nimeshaanza kufanya mazoezi mepesimepesi, ni matumaini yangu kuwa baada ya muda nitarejea uwanjani kwa ajili ya kuipigania timu yangu ili tuweze kuiondoa Simba katika nafasi ya kwanza.
“Uwezo wa kufanya hivyo upo kabisa, kikubwa ni kuhakikisha tunashinda mechi zetu saba ambazo tutacheza ikiwemo ile ya Simba baada ya hapo sisi ndiyo tutakuwa vinara wa ligi mpaka mwisho wa msimu, kwani naamini nitakuwa naibeba timu yangu kila mechi,” alisema Tambwe.
No comments:
Post a Comment