Thursday, September 14, 2017

INDIA:MASHUA YAPINDUKA NA KUSABABISHA VIFO

Watu takriban 22 wameripotiwa kufariki baada ya mashua iliyokuwa imebeba abiria hamsini kupinduka kaskazini mwa India.


Kwa mujibu wa habari,mashua hiyo ilikuwa imebeba abiria zaidi ya uwezo wake.

Ajali hiyo metokea katika mto wa Yamuna ulio maili 30 kutoka New Delhi.

Ripoti zinaonyesha kuwa wanawake wengi ndio wamepoteza maisha katika ajali hiyo.

Miili 19 imepatikana huku watu wengine 16 wakiwa wamepelekwa hospitalini.

Kuna baadhi ya abiria hawajulikani walipo mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment