Diego Costa anayelipwa mshahara wa pound 185,000 kwa wiki na Chelsea, anafikiriwa kufungiliwa shitaka la kukiuka vipengele vilivyomo katika mkataba wake, Costa ni miongoni mwa majina 25 ya wachezaji wa Chelsea watakaoshiriki EPL 2017/2018 lakini hayumo katika list ya Champions League.
Moja kati ya sababu zilizomfanya Diego Costa agome kurudi Chelsea anadaiwa kutokuwa katika mahusiano mazuri na kocha wa sasa wa Chelsea Antonio Conte, hivyo alikuwa anashinikiza kurudi Atletico Madrid kwa mkopo kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.
Hivi karibuni Diego Costa kutokana na kukosekana katika kikosi cha Chelsea kilichosafiri kwa ajili ya Pre Season Tour alipigwa faini, Costa amebakiza mkataba wa miaka miwili na Chelsea na kama akiendelea kugoma kurudi inawezekana akalazimika kulipa fidia ya kuvunja mkataba wake.
No comments:
Post a Comment