DAIMOND AZIDI KUMPANDISHA PRESHA ZARI
Siku ya September 14, 2017 mpiga picha maarufu wa Diamond Platnumz, Kifesi alipost picha ya boss wake Diamond kwenye ukurasa wake wa instagram Picha ambayo alimpiga yeye, baada ya post hiyo mzazi mwenza na mpenzi wa Diamond Platnumz, Zari the Boss Lady akakoment kwenye post hiyo kwa kuweka emoji ya kidole cha kati.
Baada ya Zari kukomenti hivyo mashabiki wakahusisha hilo na swala ambalo Diamond anadaiwa ya kuwa yupo Zanzibar na mshindi wa Big Brother mwaka 2013 anayetokea Namibia, Dilish Methew huku ikisemekana wawili hao wanatoka kimapenzi kitu kilichomfanya Zari akomenti vile kwenye picha ya kifesi aliyompost Diamond.
No comments:
Post a Comment