Mbunge Zitto Kabwe
Akizungumza kwenye mkutano na wananchi Mkoani Mwanza alipokuwa akifanya uzinduzi wa matawi ya chama hicho, Zitto amesema wameamua kufanya hivyo kwa kuwa sheria ya vyama vya siasa haimtaji rais mahali popote na iwapo ana mamlaka kisheria kuzuia kufanyika kwa mikutano ya kisiasa.
“Leo hii vyama tunahangaika haturuhusiwi kufanya mikutano, tumekubaliana tufungue kesi dhidi ya serikali ili Mahakama itoe amri kuhusiana na nani mwenye haki ya kuzuia mikutano, kwa sababu sheria ya vyama vya siasa haimtaji rais mahali popote, rais hana mamlaka ya kuagiza mikutano ya vyama isifanyike”, alisema Zitto Kabwe.
Zitto Kabwe aliendelea kwa kusema kuwa uhuru wa kidemokrasia hivi sasa unaendelea kuminywa na kuwataka wananchi wasidanganywe kirahisi kuwa muda wa kufanya siasa umeisha, kwani wakati wote ni wakati wa siasa kwa sababu hata hayo maendeleo yanaletwa na siasa pia.
“Asiwadanganye mtu yeyote, awe na cheo chochote kwamba kuna nyakati za kufanya siasa na nyakati za kufanya mandeleo. Wakati wote ni wakati wa siasa na kufanya maendeo, kwa sababu siasa ni maendeleo”, alisema Zitto Kabwe.
Mwaka 2015 baada ya Rais Magufuli baada ya kuapishwa alizuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa, akisema kuwa wakati wa siasa umeisha hivyo ni muhimu wakaacha kushabikia siasa na kujikita kwenye shughuli za maendeleo zaidi, kitendo ambacho vyama vya upinzani wamekuwa wakikilalamikia kuwanyima uhuru wa kidemokrasia.
No comments:
Post a Comment