Tuesday, August 8, 2017

TRUMP:TUTAIKABILI KOREA KASKAZINI KIVITA IKIENDELEA NA VITISHO

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Korea Kaskazini itakabiliwa kivita iwapo itatoa vitisho kwa Marekani.

Matamshi yake yanajiri baada ya ripoti ya gazeti la The Washington Post, kudai maafisa wa ujasusi ambao wanasema kuwa Pyongyang imezalisha kichwa kidogo cha kinyuklia kinachoweza kutoshea katika makombora yake.

Hii inamaanisha kwamba Korea Ksakazini inatengeza silaha za kinyuklia zinazoweza kushambulia Marekani kwa kasi ya juu zaidi ya ilivyodhaniwa.

Umoja wa mataifa hivi majuzi uliidhinisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya taifa hilo.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilikubali kuipiga marufuku Korea Kaskazini kuuza bidhaa zake nje mbali na kupunguza uwekezaji hatua iliozua hisia kali kutoka kwa Korea Kaskazini ambayo iliionya Marekani.

Mataifa hayo mawili yamekuwa yakirushiana maneno baada ya Pyongyang kufanyia majaribio makombora yake ya masafa marefu mnamo mwezi Julai, ikisema kuwa yana uwezo ya kushambulia Marekani.

Bwana Trump ameambia wanahabari siku ya Jumanne: Korea Kaskazini isitoe vitisho kwa Marekani. watakabiliwa kivita kama vile ambavyo ulimwengu haujawahi kuona.

No comments:

Post a Comment