Monday, August 21, 2017

RAIS SHEIN AAGIZA MADEREVA KUNYANG'ANYWA LESENI ZANZIBAR


Akiwa katika wilaya ya Mjini magharibi 'B' katika siku ya tatu ya Ziara yake aliyoianza juzi Ijumamosi katika mkoa wa mjini magharibi, visiwani Zanzibar, Rais Dkt Ali Mohamed Shein amewataka askari wa usalama barabarani kutumia sheria ipasavyo ikiwa ni pamoja na kunyan'ganya leseni madereva wa vyombo vya moto wanaokiuka sheria za usalama barabarani visiwani humo.

Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya magogoni kwa Mabata hadi Kijitoupele, ambapo alisema trafiki wasitegemee uwepo wa matuta barababarani utawafanya madereva wasikiuke sheria, na badala yake wazitumie kikamilifu sheria zilizopo ili kupunguza uharibifu na ajali za barabarani ambapo ametumia fursa hiyo kuwaasa askari hao kutokubali kupokea rushwa kutoka kwa Madereva waliotenda makosa.


Kwa mujibu wa Katibu mkuu Ofisi  ya Rais TAMISEMI na idara malaamu za SMZ Radhia Haroub Abdallah, amemueleza Rais Shein Mradi huo umegharimu shilingi bilioni 1.15 na kwamba kampuni jenzi ya MECCO imethibitisha kukamilisha mradi huo ndani ya miezi 2 badala ya miezi 6. 

Pia Rais Shein amezindua madarasa matatu na maktaba moja katika skuli ya msingi ya Kijitoupele yaliyojengwa na kukamilika ndani ya siku 11 kwa na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 70 chini ya kampeni ya "Mimi na Wewe" iliyoasisiwa na Ofisi ya mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Ayoub Mohamed Mahamoud 

Shughuli hizo pia ziliambatana na uwekaji jiwe la msingi katika ofisi vya CCM maskani ya tuko imara shehia ya bweleo, ambapo alihitimisha ziara hiyo ya siku tatu kwa kukagua  miradi miwili ya maendeleo ya nyumba za makazi iliyopo Fumba na Nyamazi na kuwahakikishia Wazanzibar na watanzania kwa ujumla kutokiwa na hofu kwakuwa nyumba hizo zimezingatia watu hali zote.

 Ziara hiyo ni ya kwanza kwa Rais Shein tangu achaguliwe katika uchaguzi wa marudio mwaka jana, Na ni ya tatu tangu aingie madarakani mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment