Thursday, August 3, 2017

BREAKING NEWS: NYUMBA YA SHEIKH DSM YANUSURIKA KUCHOMWA MOTO

Nyumba ya Mwenyekiti wa Taasisi ya Imam Bukhari Jijini Dar es salaam Sheikh Khalifa Khamisi imenusurika kuteketezwa kwa moto na watu wasiojulikana.

Kwamujibu wa Sheikh Khalifa Khamisi anayeishi Kinondoni, Magomeni mtaa wa Lalago, tukio hilo limetokea majira ya saa nane na dakika 3, usiku wa kuamkia leo ambapo na likadumu kwa zaidi ya nusu saa, na ilipofika asubuhi jeshi la polisi liliwasili katika nyumba hiyo kwa uchunguzi zaidi.

Jitihada za kumtafuta Kamanda za Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni zinaendelea. Licha ya kumtafuta kwa njia ya simu bila majibu


No comments:

Post a Comment