KATIBU MKUU WA BMT, MOHAMMED KIGANJA.
SIKU moja baada ya wanachama wa Simba kuridhia mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji katika klabu yao, Baraza la Michezo Tanzania (BMT), limesema linasubiri taarifa rasmi ili liweze kutoa mwongozo ndani ya klabu hiyo.
Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja, alisema taarifa za Simba kufanya mkutano huo wanazifahamu na ofisi yake ilizikaimisha kwa Msajili wa Vyama na Klabu za Michezo nchini.
Kiganja alisema kuwa anaamini viongozi na wanachama wa klabu hiyo watakuwa wamefanya uamuzi kwa kuzingatia katiba.
"BMT kwa sasa hatuwezi kusema chochote kuhusiana na kilichopitishwa katika mkutano huo wa jana (juzi), mpaka tutakapopata taarifa rasmi ya kile kilichoamuliwa na wanachama hao, mimi nimesikia kupitia vyombo vya habari ambavyo kila kimoja kimeandika kulingana na mrengo wake," alisema Kiganja.
Wanachama 1,216 kati ya 1,217 waliokutana juzi walikubali kwa kauli moja kuuza asilimia 50 ya hisa kwa mwekezaji yeyote au watu wowote watakaoungana wasiozidi watatu kwa dau la Sh. bilioni 20 wakati kwa kuanzia wanachama wote wa Simba wamepewa asilimia 10 ya hisa ambazo zina thamani ya Sh. bilioni nne.
Kiasi kingine cha hisa asilimia 40 kilichobakia ambacho thamani yake ni Sh. bilioni 16, kitauzwa baadaye kwa wadau huku ikiwekwa sharti kuwa wawekezaji walionunua hisa za awali hawataruhusiwa kununua tena.

No comments:
Post a Comment