ERASTO NYONI.
Nyoni anatua Simba akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Azam FC wakati Mohammed naye ameshamaliza mkataba na Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani ya Morogoro.
Taarifa kutoka katika klabu ya Simba zinasema kuwa kila mchezaji atasaini mkataba wa miaka miwili muda mfupi baada ya kurejea nchini kutoka Kigali, Rwanda.
"Tumewapata, naweza kusema hivi kwa kifupi," alisema kiongozi mmoja wa klabu hiyo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Mohammed, alisema kuwa tayari ameshakamilisha mazungumzo na Simba kilichobakia ni kukamilisha taratibu za kusaini mkataba.
"Kweli nimezungumza nao na kukubaliana, nikitoka Rwanda nasaini mkataba," alisema kipa huyo ambaye aliwahi pia kuwadakia mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga ya jijini.
Aliongeza kuwa anashukuru Simba kwa kuona kipaji chake na anawataka wajiandae kuona wamepata kipa mwenye kiwango cha juu.
Naye Nyoni alisema kuwa ameamua kutua Simba kwa sababu ya kukubali kumpa mahitaji yake ambayo amewaeleza.
"Yanga nilizungumza nao kule Mwanza lakini hatukukamilisha, Simba ndio walianza, lakini hapa katikati simu yangu ilinikwamisha na kuamua kusajili beki mwingine," alisema beki huyo aliyekulia katika kituo cha Rollingstone jijini Arusha.
Simba iliamua kumsajili Salim Mbonde baada ya kumkosa Nyoni siku chake kabla Taifa Stars haijaenda Mwanza kuivaa Rwanda (Amavubi) na uamuzi wa kurejea kwake unatokana na Mbonde kutakiwa na klabu moja ya Serbia.
No comments:
Post a Comment