Thursday, June 15, 2017

WASANII WAWATUPIA LAWAMA WANASIASA KUIPOROMOSHA SANAA


 Wasanii walioto changia mada katika Kongamano la tisa la Kigoda cha Mwalimu Nyerere leo Alhamisi, wamesema wanasiasa ndiyo wanaoshiriki kubadilisha lengo na mwelekeo halisi wa sanaa ya Afrika.

Wasanii waliopata nafasi ya kutoa mchango wao katika kongamano hilo ni John Kitime, Carola Kinasha, Niki wa Pili na FID Q.

Nay wa Mitego naye alikuwa miongoni mwa wazungumzaji hao, lakini mpaka sasa bado hajawasili kwenye ukumbi wa Nkurumah katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lipofanyika kongamano hilo.

Akizungumza katika kongamano hilo  lililoendelea kwa siku ya tatu mfululizo leo, msanii Niki wa Pili ambaye amesema wasanii wanatumiwa na wanasiasa kwa propaganda za kisiasa bila kujali kuwa dhima ya sanaa ni ukombozi.

Naye Fid Q amesema wasanii hushiriki katika kampeni kwa ajili ya kujipatia fedha.

 "Fedha zenyewe ni nyingi kweli zina uwezo wa kutatua baadhi ya changamoto zinazozungumzwa katika majukwaa hayo,” amesema.

Mada kuu katika kongamano hilo la Kigoda cha Mwalimu mwaka huu ni nafasi ya viongozi wa siasa katika kuanguka na kuinuka kwa maendeleo ya Afrika.

No comments:

Post a Comment