Hii sio mara ya kwanza kwa Salah kucheza katika ligi kuu nchini Uingereza kwani hapo mwanzo kabla hajahamia nchini Italia aliwahi kukipiga na timu ya Chelsea.
Mohamed Salah amesema ujio wake Liverpool ni tofauti na Chelsea kwani kipindi wakati anaenda Chelsea alikuwa bado mtotomtoto lakini sasa anajiona ni bora zaidi.
“Nina uhakika 100% kwamba kila kitu kimebadilika hadi muonekano wangu,kipindi kile nilikuwa na miaka 20 ila sasa nina 24 na nina uzoefu mkubwa zaidi tofauti na hapo mwanzo” alisema Salah.
Mkataba wa Salah na Liverpool utamfanyia kila mwisho wa wiki kuweka kiasi cha euro 90,000 huku akikabidhiwa jezi namba 11 na Firminho akipewa jezi namba 9.
Usajili wa Mohamed Salah wa euro million 39 umevunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Andy Caroll aliyesajiliwa kwa euro milion 35 mwaka 2011.Na hii ndio orodha ya usajili wa ghali ndani ya klabu hiyo.
1.Mohamed Salah (euro 39m).
2.Andy Carroll (euro 35m).
3.Sadio Mane (euro 34m)
4.Christian Benteke (euro 32.5m)
5.Roberto Firminho (euro 29m)
No comments:
Post a Comment