Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Riziki Pembe
Zanzibar/Dar. Kutokana na mvua inayoendelea Zanzibar na kuleta madhara kwa wananchi na miundombinu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imetangaza kuzifunga shule zote za Serikali na binafsi hadi hali ya hewa itakaporidhisha.Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Riziki Pembe Juma ilisema uamuzi huo umechukuliwa baada ya kuwapo tahadhari iliyotolewa kwa visiwa vya Unguja na Pemba kuhusu mvua.
Zaidi ya nyumba 1,000 zimeripotiwa kuathiriwa na mvua, baadhi zikiwa zimebomoka Unguja na Pemba tangu kuanza kunyesha mfululizo wiki moja iliyopita.
Miongoni mwa nyumba hizo, 666 zipo Pemba na 360 za Unguja katika mikoa yote mitano ya Zanzibar.
Waziri Pembe katika taarifa hiyo alisema wameamua kufunga shule ili kuwalinda wanafunzi na hatari zinazoweza kutokea kama mvua itaendelea kunyesha.
No comments:
Post a Comment