Maafisa wa Marekani wanasema manowari ya wanamaji wa Marekani imetekeleza oparesheni maalum ya 'uhuru wa ubaharia' karibu na visiwa vinavyozozaniwa vya bahari ya kusini mwa china.
Oparesheni hiyo karibu na kisiwa kimoja bandia kilichojengwa na Uchina inalenga kupinga madai yan Uchina ya kumiliki eneo hilo.
Uchina inadai umiliki wa visiwa na miamba ya baahari ya kusini mwa China.
Mataifa mengine pia yanadai umiliki wa visiwa hivyo pamoja na miamba.
Marekani inasisitiza kwamba ina uhuru wa kutekeleza oparesheni zake katika maeneo yoyote kwenye maji ya kimataifa.
Oparesheni hiyo imefanyika karibu na visiwa cha Spratley, ambapo Uchina imejenga kambi ya kijeshi, jambo ambalo limezua ghadhabu miongoni mwa mataifa jirani.
Oparesheni hiyo ni ya kwanza tangu kuanza utawala wa rais Donald Trump, na inalenga kukabiliana na majaribio ya Uchina ya kdhibiti eneo, ambalo huwa linashuhudia shughuli nyingi za ubaharia.
Kumekuwa na vita baridi kati ya Uchina na Marekani, ambapo kumekuwa na lawakma kuwa eneo hilo linageuzwa kuwa la kijeshi.
Oparesheni hiyo ya Marekani itaathiri pakubwa uhusiano wake na Uchina, hususan wakati ambapo utawala wa rais Trump unataka ushirikiano wa Beijing katika kukabiliana na vitisho vya mashambulizi ya kinyuklia ya Korea Kaskazini
No comments:
Post a Comment