Kamati
ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge la Tanzania, leo imewasilisha
bungeni taarifa za matukio mbalimbali ambazo imezifanyika kazi ikiwa ni
pamoja na kuwaita na kuwahoji wahusika kwa kukiuka kanuni za bunge nje
na ndani ya bunge hilo.
Miongoni
mwa taarifa hizo ni pamoja na ile ya kuingilia uhuru wa bunge kosa
lililofanywa na Paul Christian Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,
Alexander Mnyeti.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka bungeni, viongozi hao wate wawili wamesamehewa
kutokana na kukiri makosa yao na kuliomba radhi bunge la Tanzania.
Aidha,
Kamati ya Maadili ya Bunge imemsamehe Kiongozi wa Upinzani Bungeni,
Freeman Mbowe baada ya kukiri kutoa lugha ya kudharau mamlaka ya bunge.
Pia
Kamati ya Maadili ya Bunge imemuadhibu Mbunge Halima Mdee kutohudhuria
vikao vya Bunge la Bajeti vilivyosalia kwa kudharau mamlaka ya bunge.
Hata hivyo, Bunge limeazimia kumsamehe mbunge huyo baada ya Wabunge wa pande zote kumuombea msamaha .
Katika
hatua nyingine,Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya amepewa karipio
kali na Kamati ya Maadili ya Bunge kwa kosa la kudharau Mamlaka ya
Spika wa Bunge.
No comments:
Post a Comment