MWANAMUZIKI aliyetamba na Wimbo wa Mahaba Niue, Maua Sama ameeleza namna
ilivyo vigumu kwa wasanii wengi wa Bongo kupenya, kujitanua na
kulivuruga soko la kimataifa kutokana na changamoto nyingi ikiwemo
kuoneana wivu.
Akipiga stori na Uwazi Showbiz, mwanamuziki huyo aliweka wazi kuwepo kwa baadhi ya wanamuziki wasiopenda mafanikio ya wenzao, hivyo kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha wenzao hao wanakwama na hawajitanui kimataifa jambo ambalo limesababisha na wao pia kukwama kimataifa.
“Inahitaji jitihada za ziada kupenya kimataifa lakini pia kujipanga kwelikweli.
Wanamuziki wengi wa Bongo wanaoneana wivu na wanapikiana majungu, yaani unaweza kujikuta umeweka mipango yako vizuri ya kusonga mbele hata kwa kuongea na baadhi ya watu wa nje kufanya nao kazi lakini wao wanaharibu. Kwa hiyo hiyo ni miongoni mwa changamoto inayorudisha wasanii wengi nyuma nikiwemo mimi,” alifunguka Maua

No comments:
Post a Comment