Kiemba amesema alionekana msaliti ndani ya Simba kwa sababu viongozi wa klabu hiyo walidai alikuwa anajituma anapocheza kwenye kikosi cha timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ukilinganisha na kwenye klabu yao.
“Zilikuja shutuma kwamba najitolea sana kwenye timu ya taifa kuliko kwenye klabu, lakini watu hawajui kuna tofauti kucheza timu ya taifa na klabu. Mbinu zinazotumiwa na makocha zinatofautiana, majukumu unayopewa na kocha huyu yanatofautiana na kocha mwingine halafu wanatakiwa kujua unacheza ukiwa umezungukwa na kina nani?,” alihoji Kiemba nilipofanya nae mahojino mkoani Shinyanga.
“Hivyo ni baadhi ya vitu ambavyo vinatofautisha uchezaji wa mtu mmoja anapokuwa kwenye klabu na timu ya taifa au anapohamia klabu nyingine na hapo ndipo ubora wa mtu unakuwa unaonekana.”
“Kwa hiyo nikawa naonekana kama naihujumu timu, nikasimamishwa kimya kimya badae nikaitwa kwenye kikao tuzungumze ili tuyamalize nirudishwe kucheza lakini mimi nikakataa nikawaambia tuishie hapohapo.”
Ndio ukaanza mpango wa kutakiwa kuondoka, wakaja Azam wakanitaka kwa mkopo lakini Simba wakawa hawataki kuniachia wanataka walipwe hela, nikawa nashangaa kwanini wanataka hela wakati mwanzo walikuwa wanataka niondoke.”
“Bahati nzuri Azam wakanichukua nilikuwa nimebakiza miezi sita mkataba wangu na Simba uishe nikamaliza miezi sita Azam wakaniruhusu kuondoka nikaenda Stand United.”
Kiemba ni miongoni mwa wachezaji wachache kuwahi kucheza vilabu vitatu vikubwa vya Tanzania (Yanga, Simba na Azam) kwa nyakati tofauti, mchezaji mwingine ni Mrisho Ngasa.
No comments:
Post a Comment