Tuesday, May 2, 2017

HALIMA MDEE KUTOHUDHURIA VIKAO VYA BAJETI,"APIGWA STOP"


Mbunge wa jimbo la Kawe, Mhe. Halima Mdee amepewa adhabu ya kutohudhuria vikao vyote vya bajeti katika bunge linaloendele hivi sasa Dodoma kufuatia Mbunge huyo kubainika kuwa alitukana bungeni, lakini Kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani amesamehewa.

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imemtia hatiani Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani, Mhe. Freeman Mbowe kwa kudharau mamlaka ya spika na kumsamehe kosa lake hilo kwa kile lichosema kuwa lilikuwa ni kosa la kwanza kwa kiongozi huyo kufanya.

Akisoma uamuzi huo, mjumbe wa kamati, Almasi Maige amesema Bunge lijadili na kutoa uamuzi kwa kiongozi huyo kusamehewa kwa sababu ni kosa la kwanza na aliitikia wito bila usumbufu na aliomba radhi, hivyo bunge limeazimia kumsamehe.

Mambo yamekuwa magumu kwa kwa upande wa Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee ambapo bunge limeazimia mbunge huyo kutohudhuria vikao vya bunge la bajeti vyote vinavoendelea sasa kwa kosa lake la kumtukana Spika na Mbunge akiwa bungeni.

Halima Mdee amesimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge la bajeti kufuatia lugha ya matusi aliyotoa bungeni siku ya Uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki uluiofanyika tarehe 4 mwezi 4 2017 bungeni, hata hivyo Mbunge huyo aliomba radhi bungeni kwa kitendo hicho na kuwataka Watanzania kumsamehe.
 

No comments:

Post a Comment