Saturday, May 6, 2017

BRAZIL WAPAA TENA KILELENI VIWANGO VYA FIFA DUNIANI

Shirikisho la kandanda Ulimwenguni Fifa limetoa orodha mpya ya ubora wa viwango vya soka ulimwenguni.

Nchi hiyo kwa miaka ya karibuni ilikuwa ikisuasua kwenye soka hali iliyosababisha washindwe kufanya vizuri kwenye list hiyo ya viwango vya ubora duniani.

Kwa mujibu wa list mpya, Brazil ni vinara kwa nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Argentina nafasi ya pili,nafasi ya tatu ni Ujerumani,nafasi ya Nne ni Chile, nafasi ya tano ni Colombia ,nafasi ya sita ni Ufaransa,nafasi ya saba ni Ubeligiji, nafasi ya nane ni Ureno ,nafasi ya tisa ni Switzerland na nafasi ya kumi ni Hispania.

Kwa upande wa Afrika Misri bado ni vinara ikiwa katika nafasi ya 19 Ulimwenguni, na orodha nyingine ya ubora Duniani itatoka tena Juni Mosi.

No comments:

Post a Comment