Thursday, April 20, 2017

WAPINZANI WAWACHANA LIVE MAWAZIRI

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa  na mbunge wa viti maalum (Chadema), Upendo Peneza wakichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais (Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora) kwa mwaka 2017/2018 mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi 

Dodoma. Kufanya kazi kwa hofu kumesebabisha mawaziri na watendaji kupooza, imeelezwa.
Wabunge wa upinzani walitumia siku ya jana kuichambua Serikali, wakati wakichangia hotuba za bajeti za Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2017/18.
Tamisemi inaomba kuidhinishiwa Sh6.5 trilioni, huku Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ikiomba kuidhinishiwa Sh821 bilioni.
Katika mjadala huo, Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa alisema tangu mwaka 1980 hadi 2010, Afrika pamoja na rasilimali ilizonazo, imepoteza Dola 1.4 trilioni za Marekani kutokana na uongozi mbovu.

“Mojawapo ya sababu ni kwa kuwa hakuna mwendelezo kwa viongozi wanapobadilishana madaraka. Katika awamu ya tano kumekuwa na changamoto kubwa ambazo takwimu hizi zinashabihiana kuwa tutaendelea tena kupoteza mali tulizonazo kutokana na uongozi,” alisema mchungaji huyo wa Kanisa la Vineyard.

No comments:

Post a Comment